(Yoro Diallo) Msomi wa Mali: Pendekezo la GCI laweka mfumo muhimu kwa ajili ya kuhimiza kufunzana kwa usawa kati ya staarabu anuwai

Par Prof. Yoro DIALLO, Chercheur Principal/Directeur du Centre d’Etudes Francophones, Directeur du Musée Africain et du Musée des Echanges Chine-Afrique, Institute of African Studies, Zhejiang Normal University

Source:https://swahili.cgtn.com/2026/10/30/ARTI1793328060685452


Msomi wa Mali na mjumbe wa Jopo la Majaji la Tuzo ya “Orchid Awards” Prof. Yoro Diallo amesema, katika mazingira ya sasa ya kimataifa ambayo changamoto na hatari mbalimbali zimechangamana, mivutano ya siasa za kijiografia inazidi kupamba moto, pengo la maendeleo linazidi kupanuka na mgawanyo wa kiutamaduni unazidi kuonekana, umuhimu wa mazungumzo kati ya staarabu tofauti yamejitokeza zaidi katika zama hizi. Pendekezo la Ustaarabu Duniani (GCI) lililotolewa na China linatetea uanuwai wa staarabu, linazichukulia staarabu anuwai kuwa hazina ya pamoja ya binadamu, na wala sio kizuizi cha ushirikiano.


Prof. Yoro Diallo amesisitiza kuwa mshikamano wa binadamu haumaanishi kuwa staarabu zote zitasawazishwa, na kwamba hakuna ustaarabu mmoja pekee unaoweza kutatua peke yake masuala yote yanayoikabili dunia. Amesema ni muhimu kuachana na wazo la ukuu wa ustaarabu fulani, badala yake staarabu tofauti zinapaswa kufanya mazungumzo kwa usawa katika msingi wa kuheshimiana. Kufunzana kati ya staarabu kunalenga kuhimizana na kukamilishana, na hakutafuta sifa maalum za kila moja.


Msomi huyu amesema, mawasiliano ya kiutamaduni ni kiungo kinachounganisha mioyo ya watu, na Tuzo ya “Orchid Awards” inawatambua na kuwatia moyo watendaji wa kuhimiza mazungumzo kati ya staarabu. Anaona jambo muhimu zaidi kwa mawasiliano ya kiutamaduni ni ushiriki wa umma, ambapo binadamu wanapaswa kufunzana, kukusanya nguvu za staarabu anuwai na kukuza ustawi wa pamoja kwa wote.


Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn