Mwaka 2008 Kitivo cha Utafiti wa Afrika kilianza kupokea wanafunzi wa shahada ya uzamili na wanafunzi kutoka nchi za nje katika kozi ya Historia ya Dunia na Ulinganishi wa Elimu. Kozi ya Historia ya Dunia huwaandaa wanafunzi ambao wana msingi imara wa natharia na ujuzi wa historia ya dunia na utafiti wa Afrika, tena wanaweza kufanya kazi ya natharia na ya uhalisi katika taasisi za mafundisho, za utafiti na makampuni mbalimbali. Kozi ya Ulinganishi wa Elimu huwaandaa wanafunzi ambao wana msingi imara wa natharia na ujuzi wa ulinganishi wa elimu na taaluma ya Afriika, tena wanaweza kufanya kazi ya natharia na ya uhalisi katika taasisi za mafundisho, za utafiti na makampuni mbalimbali. Mpaka sasa, Kitivo cha Utafiti wa Afrika kimejenga uhusiano wa kitaaluma pamoja na vyuo vikuu zaidi ya 20 vya Afrika. Baada ya wanafunzi wa shahada ya uzamili wa kitivo kumaliza masomo ya lazima hapa nchini, baadhi ya wanafunzi hodari watachaguliwa kusomea vyuo vikuu maarufu vya Ulaya, Marekani, Japani au Afrika. Wakati kitivo kinapochagua watafiti, wanafunzi hodari hupewa kipaumbele.


Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn