Kitivo cha Utafiti wa Afrika cha Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang kina taasisi nne, vituo vitatu na Jumba moja la makumbusho.


Taasisi ya Utafiti wa Siasa ya Afrika na Uhusiano wa Kimataifa

Wako watafiti wanane. Miongoni mwao kuna Maprofesa wawili, Mtafiti Msaidizi mmoja na Wahadhiri watano.Wao hushughulikia utafiti wa siasa ya Afrika na uhusiano kati ya China na Afrika katika enzi hii. Mpaka sasa wamepata miradi mingi ya Mfuko wa Sayansi ya Jamii wa Taifa, ya Wizara ya Elimu na ya Wizara ya Mawasiliano ya China. Na utafiti unagusia uhusiano kati ya China na Afrika, diplomasia kati ya Afrika na nchi kubwa, mgogoro wa Darfur nchini Sudan, jumuiya zisizo za serikali za Afrika, utafiti wa kila nchi na sekta nyingine.


Taasisi ya Utafiti wa Uchumi wa Afrika

Wako watafiti watatu. Na miongoni mwao kuna Wahadhiri wawili na Mhadhiri Msaidizi mmoja. Taasisi hiyo ni taasisi muhimu itakayoingiza watafiti hodari katika siku za mbele. Wao hushughulikia utafiti kuhusu uchumi wa Afrika katika enzi hizi na uhusiano kati ya China na Afrika, vielelezo vya maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika, uchumi wa kila nchi, uwekezaji wa China barani Afrika na ukwepaji wa hatari n.k.


Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya Afrika

Wako watafiti watano. Na miongoni mwao kuna Profesa mmoja, Maprofesa Wasaidizi watatu na Mhadhiri mmoja. Wao hushughulikia utafiti kuhusu elimu ya Afrika na ushirikiano wa elimu kati China na Afrika. Ikishirikiana na kituo cha msaada wa elimu kwa nje cha Wizara ya Elimu, inahimiza mafunzo kwa Afrika kwa kupitia utafiti, na kuongoza utafiti kwa mafunzo.


Taasisi ya Historia na Utamaduni wa Afrika

Wako watafiti watatu, na wote wamepata shahada ya juu. Wao hushughulikia utafiti wa historia, dini, utamaduni na taaluma ya binadamu.


Maktba ya vitabu vya Afrika

Eneo la maktaba hii ni mita za mraba zaidi ya 600. Mazingira yake ni mazuri, na kuna zana za kisasa za kila aina. Sasa kinahifadhi zaidi ya aina 5000 za vitabu vya utafiti na aina 34 za majarida ya lugha ya Kiingereza. Lengo la maendeleo ni kuwa kituo cha taaluma cha vitabu vya Afrika chenye umaalum wa kichina na kiwango cha kimataifa.


Kituo cha Uenezi wa Sanaa ya Kiafrika

Afrika ni bara lenye mandhari nzuri na sanaa maalum. Kutokana na mpango wa ujenzi wa kitivo, njia za sanaa za taaluma ya binadamu na mawasiliano ya habari zitatumiwa kama njia za kupanua upeo wa macho wa utafiti, kuboresha njia za utafiti, kutengeneza video zinazoonesha mandhari ya Afrika na utamaduni wa Waafrika, mahojiano ya watu wanaohimiza uhusiano kati ya China na Afrika n.k.


Kituo Kinachoshughulikia Maswali Kuhusu Biashara na Uwekezaji Barani Afrika

Kutokana na matunda ya utafiti wa Afrika ya kitivo, kituo hiki kimelenga kuwa kituo kilicho wazi ambacho kinashughulikia maswali kuhusu biashara. Kitatoa majibu ya maswali kuhusu habari mbalimbali na mafunzo ya kila aina kwa jamii ili kuhudumia maendeleo ya jamii na uchumi ya kanda za Jiangsu na Zhejiang.


Jumba la Makumbusho ya Afrika

Jumba la Makumbusho ya Afrika ni jumba la makumbusho la kwanza barani China ambalo linashughulikia Afrika maalum. Humo jumbani kuna vitu vya sanaa, vya mila na desturi, vyombo vilivyotumiwa katika maisha ya watu wa kale wa Afrika n.k. Jumba hili linatumiwa kuhimiza mawasiliano kati ya China na Afrika na maandalizi ya wanafunzi.


Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn