Liu Hongwu

Mwanazuoni wa Changjiang (aliteuliwa na Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Watu wa China), mwanazuoni wa Qianjiang (Kigoda cha Taaluma cha Serikali ya Jimbo la Zhejiang), mkurugenzi wa IASZNU, msimamizi wa wanafunzi wa shahada ya udaktari, makamu mwenyekiti wa Chama cha Kichina cha Masomo ya Kihistoria ya Afrika, mwanachama wa Chama cha Kichina cha Masomo ya Kiasia na Kiafrika, mwanachama wa Chama cha Kichina cha Masomo ya Mashariki ya Kati, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo ya Kiafrika Chuo Kikuu cha Yunnan. Liu Hongwu alipata kuwa mwanazuoni wa kuzuru katika Chuo Kikuu cha Lagos Nigeria na Chuo Kikuu cha Dar es salaam Tanzania, amekamilisha miradi kadha wa kadha iliyofadhiliwa na Mfuko wa Serikali wa Sayansi ya Jamii. Amechapisha majarida ya kitaaluma zaidi ya 100 na vitabu zaidi ya 10, na ameshinda tuzo mbalimbali katika ngazi ya kitaifa kwa mafanikio yake ya kufundisha.

                                        Simu: +86-579-8228-6081, Barua pepe: liuhongwu@zjnu.cn


  Wang Heng

Katibu wa Chama, naibu mkurugenzi na Profesa wa Taasisi ya Masomo ya Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University. Anapendelea kufanya tafiti zinazohusiana na mitaala, mbinu za ufundishaji, itikadi na elimu ya kisiasa pamoja na uongozi wa kitaaluma.Wang Heng amechapisha zaidi ya majarida 10 na ametekeleza miradi kadha wa kadha katika ngazi ya jimbo iliyofadhiliwa na Wizara ya Elimu. Tuzo alizowahi kushinda ni pamoja na Tuzo ya Mafanikio ya Kufundisha ya Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University; tuzo ya kwanza akiwa kama kiongozi wa mradi na tuzo ya pili akiwa kama mwanachama wa kundi. Pia amewahi kushinda tuzo ya Elimu ya Jimbo la Zhejiang.

Simu: +86-579-8228-7057, Barua pepe: wh2516@zjnu.cn



  Gu Jianxin

Naibu mkurugenzi Idara ya Masuala ya Kigeni ya Serikali ya Jimbo la Zhejiang na naibu mkurugenzi wa IASZNU, Profesa, Shahada ya Uzamivu (PhD) katika filosofia, mwanachama wa Chama cha Kichina cha Masomo ya Kihistoria ya Afrika na ni mwalimu mashuhuri kitaifa. Gu Jianxin amewahi kutembelea nchi za Afrika ikiwemo Afrika Kusini pamoja na Moroko, na anajihusisha zaidi na tafiti zinazohusu Afrika hususan elimu ya juu pamoja na uongozi wa masuala ya kielimu katika ushirikiano wa China na Afrika. Gu Jianxin ametekeleza miradi kadha wa kadha katika ngazi ya jimbo na amechapisha zaidi ya majarida 20 pamoja na vitabu vitano.

                                        Simu: +86-579-87050305, Barua pepe: jxgu2003@zjnu.cn


  Chen Mingkun

Naibu mkurugenzi na Profesa wa Taasisi ya Masomo ya Kiafrika Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University, msimamizi wa wanafunzi wa shahada ya uzamili, Shahada ya Uzamivu ya Filosofia (PhD) katika Elimu. Anapendelea kufanya tafiti zinazohusu elimu ya ufundi pamoja na elimu ya juu barani Afrika. Dk. Chen Mingkun amechapisha majarida mengi katika Mapitio ya Elimu Linganishi, Masomo katika Elimu ya Kigeni n.k. Monografi alizowahi kuchapisha ni Elimu ya Juu Ethiopia pamoja na Maendeleo Endelevu ya Elimu ya Ufundi wakati wa kipindi cha Mabadiliko ya Uchimi wa China.

Simu: +86-579-82287069, Barua Pepe: sdchen@zjnu.cn

Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn