Msomi wa Mali: Fikra ya Xi Jinping kuhusu Usoshalisti wenye sifa maalum za China katika zama mpya yaongoza maendeleo yenye ubora wa ushirikiano kati ya China na Afrika
Source:https://swahili.cgtn.com/2026/07/09/ARTI1783581966225990
Mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa Mali Prof. Yoro Diallo anaona, Fikra ya Xi Jinping kuhusu Usoshalisti wenye sifa maalum za China katika zama mpya si kama tu inaiongoza China kufanikisha muujiza wake wa maendeleo kuelekea kuwa nchi ya kisasa, bali pia imetoa mwongozo wa kinadharia na mfano wa kiutendaji katika kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika na kuisaidia Afrika kutimiza maendeleo kwa kujitegemea.
Prof. Diallo, ambaye ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amebainisha kuwa chini ya mwongozo wa fikra ya Xi Jinping, China siku zote imekuwa ikifuata mtazamo wa udhati, matokeo halisi, urafiki na nia njema wakati wa kushughulikia masuala ya Afrika, imeendelea kuimarisha uhusiano wa washirika wa kimkakati wa hali zote kati ya pande hizo mbili, na kuusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika kuingia katika hatua mpya ya kujenga kwa pamoja Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakbali wa Pamoja katika Zama Mpya. Amesema, mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwaka 2024 umeweka dira ya China na Afrika kuelekea usasa kwa pamoja, ambapo ulitoa sera ya ushuru sifuri kwa Afrika iliyoanza kutekelezwa Mei Mosi mwaka huu, hatua ambayo imepanua kwa kiasi kikubwa njia za kibiashara kwa bidhaa za Afrika kuingia kwenye soko la China, na kuleta manufaa halisi kwa ukuaji wa uchumi wa Afrika.
Prof. Diallo amesema, uzoefu wa China katika nyanja za uwekaji wa mipango ya kimkakati ya muda mrefu, ujenzi wa miundombinu, mapambano dhidi ya umaskini, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na usimamazi wenye ufanisi wa juu, unaendana kwa kiasi kikubwa na mahitaji ya Afrika katika ujenzi wa usasa, na unastahili kuigwa na mataifa ya Afrika kwa kuzingatia hali halisi ya nchi zao.
