Msomi wa Mali: Sera ya ushuru sifuri ya China ni alama ya maendeleo ya mtindo wa ushirikiano kati ya China na Afrika
Source:https://swahili.cgtn.com/2026/05/29/ARTI1780037990092246
Msomi wa Mali Prof. Yoro Diallo hivi karibuni amesema, sera ya China ya kusamehe ushuru kwa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi nayo, ni moja ya matukio muhimu zaidi kwenye maendeleo ya mahusiano ya kimataifa na uhusiano kati ya China na Afrika katika zama hii, na ni hatua inayoonesha mshikamano halisi wa kivitendo wa China kwa Afrika.
Prof. Diallo, ambaye ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema katika wakati huu ambapo mvutano wa kibiashara duniani unazidi kuongezeka, hatua za kujilinda kibiashara zinazidi kushamiri na mgawanyiko kwenye minyororo ya usambazaji unazidi kupanuka, sera ya ushuru sifuri ya China is kama tu inawakilisha fursa muhimu za kibiashara na ufunguaji mlango wa kihistoria, bali pia imetoa ufunguaji wa kimkakati kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Afrika na China.
Mtaalamu huyu anaona, China inajitambulisha kuwa mtetezi wa biashara huria na ushirikiano wa Kusini-Kusini. Kwa nchi nyingi za Afrika, hatua hiyo imetoa njia mbadala ya ushirikiano wa maendeleo inayotoa kipaumbele katika kuboresha miundombinu, kukuza viwanda na kuhimiza muunganiko wa kiuchumi.
