Msomi wa Mali: Mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika yaunda upya uhusiano wa pande hizo mbili katika muktadha wa utaratibu wa pande nyingi
Source:https://swahili.cgtn.com/2026/04/29/ARTI1777445504593608/
Msomi wa Mali Profesa Yoro Diallo hivi karibuni amesema mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika yamezidi kuchukua nafasi muhimu katika mipango ya utendaji iliyopitishwa katika mikutano ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na mawasiliano hayo ya karibu yaliyofanyika kwa mitindo anuwai, yamehimiza ujenzi wa nafasi isiyo na kifani ya mazungumzo kati ya tamaduni, na kuunda upya uhusiano kati ya China na Afrika katika muktadha wa utaratibu wa pande nyingi.
Prof. Diallo, ambaye ni mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema katika mwaka 2026 ambao umewekwa kuwa Mwaka wa Mabadilishano ya Watu na Watu kati ya China na Afrika, shughuli mbalimbali kubwa za kiutamaduni zinazofanyika China na Afrika kwa uhakika zitatoa mchango mkubwa katika kuzidisha maelewano na kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili.
Prof. Diallo amependekeza kuwa China na Afrika zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni kwa kukumbatia sayansi, teknolojia na ubunifu, hasa kupitia simulizi za kidijitali na kujifunza kupitia mtandao, ili kufanya uhusiano wa pande mbili uwe karibu zaidi.
