Msomi wa Cameroon: Mafanikio ya filamu ya uhuishaji ya “Nezha 2” ya China yaweka mfano mzuri wa jinsi ya kueneza na kunufaika na utamaduni wa jadi

Source: https://swahili.cgtn.com/2025/04/29/ARTI1745913774276191

 Akizungumzia filamu hiyo, msomi wa Cameroon na mkurugenzi wa Kituo cha Filamu na Televisheni cha Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Dkt. Taling Rodrigue, amesema mafanikio ya filamu hiyo yameweka mfano mzuri wa jinsi ya kueneza na kunufaika na utamaduni wa jadi, ambao pia unastahili kuigwa na watengeneza filamu wa Afrika. Haya siyo tu ni mafanikio ya filamu hiyo ya Kichina, bali pia ni onyesho lingine lenye mwangaza wa kujiamini kwa utamaduni wa China. Kutoka kuibuka kwa “Nezha 1 ” iliyoonyeshwa mwaka 2019 hadi “Nezha 2” inayopata mafanikio mapya, mfululizo wa filamu hii ya uhuishaji inayosimulia hadithi ya utamaduni wa jadi wa kichina, kupitia kujihusisha na thamani za kisasa na matumizi ya teknolojia ya ngazi ya juu, inaonyesha nguvu kubwa ya utamaduni wa China katika dunia ya leo.

 Dkt. Rodrigue amesema, ingawa bado hakuna ratiba halisi ya filamu hiyo kuoneshwa katika nchi za Afrika, lakini mpango wa uzinduzi wa filamu hiyo unahusisha kanda nyingi, inamaanisha kuwa haitachukua muda mrefu kwa watazamaji wa Afrika kuweza kuburudika na filamu hiyo katika sinema. Ameongeza kuwa kutokana na mafanikio makubwa iliyoyapata katika masoko mengine ya kimataifa, filamu hiyo ya “Nezha 2” pia inatarajiwa kufuatiliwa na kukaribishwa na watazamaji wa Afrika.



Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn