Makubaliano ya Jumuiya za Washauri Bingwa ya Afrika na China kuhusu Kukuza Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (Muhtasari) (Makubaliano ya Dar es Salaam ya Afrika-China)

Dunia inakabiliwa na changamoto leo, pia ina matumaini ya amani ya maendeleo. Ni muhimu kutoa hekima na kufikia mwafaka katika nyanja ya maarifa na mawazo, kwani jamii ya wanadamu inahitaji utegemezi zaidi wa pande zote. Kama wanachama muhimu wa Kusini mwa Dunia, Afrika na China zina jukumu la kihistoria la maendeleo na ufufuo ili kunufaisha watu wao. Wanapaswa kushiriki katika mifumo ya utawala wa kimataifa, kukuza ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi zote ili kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Mutakabali wa Pamoja. Kwa hiyo, wakati wa Mkutano wa 13 wa Kongamano la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika, tumefikia mwafaka na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo, ubadilishanaji wa maarifa, mwafaka wa kiitikadi na ustawi wa kiutamaduni kwa kuzingatia kanuni za kuheshimiana, mshikamano, ushirikiano, uwazi na ustawi wa pamoja.

1. Tunatoa wito kwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo na kuchunguza njia huru, zinazozingatia watu, kuheshimiana na kujifunza kwa pamoja. 

Tutetee maadili ya pamoja ya amani, maendeleo, haki, demokrasia na uhuru kwa binadamu wote na kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia. Tunaunga mkono nchi zote kuchunguza mfumo wa ujenzi wa mambo ya kisasa kulingana na sifa za kiutamaduni na mahitaji ya maendeleo, kuimarisha mazungumzo ya kistaarabu badala ya mizozo, na kubadilishana uzoefu wa utawala. Tutashika kanuni kwamba maendeleo ni kwa ajili ya wananchi, yanawategemea wananchi, na matunda yake yanatakiwa kuwanufaisha wananchi ili kulinda haki ya kila mtu ya kutimiza maisha bora.

2. Tunatoa wito wa kujenga mfumo wa dunia wa nchi nyingi wenye usawa na wenye utaratibu ili kuwezesha maendeleo ya pamoja.

Tunatetea demokrasia zaidi ya mahusiano ya kimataifa, kuongeza uwakilishi na sauti ya nchi zinazoendelea katika mfumo wa kimataifa, na kurekebisha kwa wakati udhalimu wa kihistoria ulioteseka Afrika. Tunaheshimu na kutetea mamlaka ya kitaifa, uadilifu wa eneo na haki ya maendeleo ya kila nchi. Zaidi ya hayo, tutaboresha ugawaji wa rasilimali za kimataifa, kushughulikia usawa katika maendeleo kati na ndani ya nchi chini ya Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, ili nchi zote, kubwa kwa ndogo, zenye nguvu kwa dhaifu, tajiri kwa maskini, ziweze kufurahia fursa sawa za maendeleo.

3. Tunatoa wito wa kuendeleza utandawazi wa kiuchumi wa kuzishirikisha na kuzinufaisha nchi zote ili kugawana faida za maendeleo.

Tumejitolea kuimarisha utawala wa kiuchumi duniani, kuondoa vikwazo vya biashara na uchumi, na kuanzisha minyororo ya kimataifa ya sekta na ya ugavi unaostahimili, unaojumuisha, na yenye ufanisi zaidi. Tunaunga mkono nchi zote zikiwemo za Afrika ziongeze faida zao za kulinganisha, kuendeleza kiwango cha viwanda na kilimo cha kisasa ili kushiriki katika mgawanyo wa sekta za kimataifa kwa kina, na kutoa mchango katika kukuza mzunguko wa uchumi wa kimataifa, ukuaji wa uchumi wa kimataifa, na ustawi wa watu wote.

4. Tunatoa wito wa kuhimiza mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa ili kuziba pengo la maendeleo.

Tunakubali kuongeza mtaji kwa benki za maendeleo za pande nyingi kama vile Benki ya Dunia (WB), ili kuboresha hali zao za kifedha na kukuza uwezo wao wa kuchanga fedha. Pia tunakubali kutoa misaada zaidi ya kupunguza umaskini na maendeleo kupitia zana za kuchanga fedha kwa msingi wa kuheshimu sera, falsafa na mahitaji halisi ya wahusika wote. Kulingana na kanuni ya kuzingatia ipasavyo haki, tutaongeza haki za umiliki wa hisa, upigaji kura za masoko yanayoibukia na nchi zinazoendelea katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Tutaanzisha kiti cha tatu cha mkurugenzi mtendaji kwa nchi za Afrika, na kuzingatia maslahi ya nchi zenye maendeleo duni katika mgao wa Haki Maalumu ya Kubadilisha Pesa (SDR).

5. Tunatoa wito wa kupatana na mapendekezo ya kimataifa na mipango ya kitaifa ili kuimarisha kamba za maendeleo endelevu za hali ya juu.

Chini ya mifumo ya Ajenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”(BRI) na nyinginezo, tumejitolea kuimarisha muunganisho wa miundombinu na mtiririko huru wa vipengele vya uzalishaji kulingana na mipango ya maendeleo ya kila nchi. Tunakuza maendeleo ya nishati safi, teknolojia ya habari, teknolojia za juu katika nyanja nyingi kama vile anga ya juu hatua kwa hatua. Tunazingatia kanuni ya majukumu ya pamoja lakini tofauti (CBDR) katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa na kukuza maendeleo ya kijani.

6. Tunatoa wito wa kuamsha maendeleo ya ndani kupitia masoko yenye ufanisi na serikali inayobeba jukumu.

Tunatetea uendelezaji wa utawala bora, usioharibika na unaozingatia sheria, kuboresha udhibiti wa mpango mkuu wa taifa na huduma za umma, kuchochea uhai wa soko ili kuharakisha mchakato wa viwanda na mchakato wa kilimo cha kisasa barani Afrika. Nchi zote zinapaswa kuimarisha uratibu wa sera za kiuchumi na upatanishi wa sheria tofauti, kurahisisha na kuwezesha zaidi biashara na uwekezaji, kulinda haki halali na maslahi ya makampuni, na kuongoza na kuhimiza mifumo mipya ya kuchanga fedha kama vile ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, ujenzi wa uwekezaji-ujenzi-uendeshaji, na uratibu wa mkopo na uwekezaji ili kuongeza ukwasi na ufanisi wa matumizi ya fedha.

7. Tunatoa wito kwa kuzingatia vitisho vya usalama vya kawaida na visivyo vya kawaida ili kuunda mazingira salama ya maendeleo.

Tunatoa wito wa kuthamini masuala halali ya usalama ya nchi zote, kutatua migogoro kupitia mazungumzo na mashauriano, na kujitahidi kuepuka vita, migogoro, ugaidi, magonjwa, au mtego wa ulinzi unaozuia maendeleo. Tunaamini kwamba utekelezaji wa Pendekezo la Usalama wa Dunia ungechangia kupatikana kwa amani na usalama duniani kote. Tunahimiza jumuiya ya kimataifa kusuluhisha mizozo kwa njia za busara na amani na kuzingatia kwa kiasi kikubwa mateso ya watu walioathiriwa na migogoro. Kuhusu msukosuko wa kifedha, tunaongeza juhudi za kuimarisha ushirikiano wa usalama wa kiuchumi na kifedha, kufungua njia zenye ufanisi na uthabiti za ulifi wa kimataifa, na kupanua ulifi kati ya nchi mbili kwa fedha za kieneyji na aina mbalimbali za akiba za fedha za kigeni. Tutachunguza uanzishwaji wa wakala wa kimataifa wa kutathmini viwango vya mikopo wenye haki chini ya mifumo ya ushirikiano kama vile Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), BRICS na nyinginezo.

8. Tunatoa wito wa kuhimiza kupitishwa kwa hatua za vitendo na madhubuti zaidi za kukuza ugawanaji wa maarifa.

Tunahimiza kwa pamoja utekelezaji wa Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia na kuimarisha kufundishana kwa kiustaarabu kati ya Afrika na China. Kwa maana hii, tunatetea na kuhimiza kuanzishwa kwa mtandao wa miungano ya jumuiya za washauri bingwa, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa jumuiya za washauri bingwa na vyombo vya habari. Tunalenga kuanzisha utaratibu wa mawasiliano wenye hali ya juu wa Muungano wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika na kuimarisha mawasiliano ya elimu, sayansi na teknolojia, afya, utamaduni na sanaa, na kushiriki katika diplomasia ya jiji. Tunatoa wito wa kutekeleza Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu Ukuzaji wa Vipaji kukuza rasilimali watu wenye ujuzi wa hali ya juu, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Dunia na kukuza sauti zetu katika masuala ya kimataifa.


Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn